Seventh-Day Adventist Church

IGOMA SDA CHURCH Kanisa makini kwa matunzo ya kiroho

Menu
Add a Slideshow to see your custom images here

Home




Mpendwa mgeni uliyetutembelea, tunapenda kukukaribisha kwa moyo wa ukunjufu kupitia kurasa za tovuti hii ili ujiongezee maarifa na habari muhimu za kukusaidia katika jitihada zako za kujiendeleza kiakili, kimwili, kiroho, na kijamii. Tunafanya kila tuwezavyo pia kukukutanisha na Yesu Kristo rafiki yako aliyekufia na ambaye hivi karibu yuaja kukuchukua kwenye makao ya amani. Kanisa la Igoma ni Kanisa la Waadventista wa Sabato linalopatikana kijiji cha Igoma kandokando ya njia itokayo Isyonje kwenda Makete katika Mtaa wa Swebo na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Tunakukaribisha tena na tena na kukuomba uwaalike wengine kututembelea.
Asante na Mungu akubariki sana